Jumatatu, 23 Machi 2015

Zitto kabwe Ataja sababu 5 za Kujiunga na ACT.

Zitto Kabwe Ataja Sababu 5 Za Kujiunga ACT......Azoa Wabunge 10 Fasta, Vigogo Lukuki wa CCM na CHADEMA Wachukua Kadi za Chama Hicho.

Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, amesema atafanya kazi kukijenga chama  cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) kwa kukipaisha kama alivyofanya kazi akiwa ndani ya Chadema.
 
Amesema akiwa kiongozi Chadema kwa miaka zaidi ya 20 alifanya kazi ya kukijenga chama na kuhakikisha kinatoka kuwa na wabunge wanne na sasa kimepanda na kuwa na wabunge 48.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Zitto alizitaja sababu tano zilizomfanya ajiunge na ACT-Tanzania ikiwamo kuvutiwa na msingi mama wa chama hicho wa kuweka mbele masilahi ya Taifa.
 
“Nataka kuwakumbusha wakati napewa uongozi huko nyuma nilishiriki kujenga chama ambacho kina wabunge wanne tu na kuna wakati tukienda kwenye mikutano tunakuta watu 20, lakini tulifikisha hadi wabunge 48.
 
“Na mimi ni mchapa kazi na sasa nimeamua kuingia kufyeka pori na nitalifyeka pori na tukikutana Novemba tutakuwa na majibu ya maneno yangu…,” alisema Zitto.
 
Akizitaja sababu tano za kujiunga na ACT-Tanzania alisema katu hatorudi nyumba kupambana kwa ajili ya rasilimali za Taifa na watu wake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha nchi inakuwa katika misingi ya uadilifu na uwajibikaji kwa umma.
 
“Nimekuwa nikipigania uzalendo kwa nchi yangu tangu nilipoanza siasa na nimekuwa nikiweka mbele masilahi ya Taifa dhidi ya kitu kingine chochote,” alisema Zitto.
 
Sababu ya pili unatokana na chama hicho kuwa pekee kinachokubaliana na itikadi ya ujamaa na kinaamini katika falsafa ya Nyerere iliyo na lengo la kurudisha nchi katika misingi iliyoasisi taifa.
 
Kutokana na hali hiyo, Zitto alisema anaamini kuwa ACT itasimama katika misingi ya uadilifu na kimeweka miiko na maadili ya viongozi katika kuhakikisha viongozi wa chama hicho wanatakiwa kukubaliana nayo kwa kusaini.
 
“Katika miaka yangu ya ubunge nimekuwa nikipigania uwajibikaji na uwazi jambo ambalo ninaliamini kwa moyo wangu kwenye utumishi wangu kwa umma.
 
“Nimefurahi kwamba kati ya misingi 10 ya ACT, uwajibikaji na uwazi ni misingi ambayo naamini inatokana na utumishi wa umma na suala la uwazi limekuwa sehemu ya jina la chama hicho hivyo kwangu ACT ni nyumbani katika siasa na katika utumishi wa umma,” alisema Zitto.
 
Zitto alisema amejiunga ACT kwa sababu amekubaliana na imani yao ya kujitegemea, bidii, umakini na weledi katika kazi kuwa ndiyo msingi wa maendeleo.
 
Sababu nyingine aliyotoa ni kukubaliana na imani ya ACT kwamba umoja ni ngao muhimu katika ujenzi wa taifa na Afrika kwa ujumla.
 
Alisema kwa sababu hiyo ameona upo umuhimu wa kurudisha nchi katika misingi iliyoliasisi taifa.
 
“Lazima tuirudishe nchi katika heshima ya uongozi wa Bara la Afrika hivyo naahidi kufanya kazi na makundi yote, wanaoamini katika siasa safi na siasa za hoja, tunataka kufungua kurasa mpya wa siasa nchini."
 
Usaliti
Akizungumzia kuhusu wanaomtuhumu kufanya usaliti, Zitto alijibu kwa kutumia nukuu za Rais wa kwanza wa Ghana, Kwame Nkurumah akisema haangalii nyuma tena bali anaangalia mbele.
 
“Naombeni mjaribu kufumba macho yenu mjiulize ni mbunge gani katika Bunge hili ambaye ametoa hoja ambazo zilikitikisa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 
“Mara mbili nimetoa hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, taarifa yangu wakati ule nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), mara mbili nimeng’oa mawaziri wa CCM, mwaka 2011 mawaziri wanane.
 
“Juzi juzi katika suala la Escrow nimewang’oa mawaziri watatu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali hivyo, swali kama hilo la usaliti lilitakiwa kupewa wale ambao wako bungeni na hawafanyi kazi ya kuiwajibisha serikali si kwa mtu ambaye maisha yake yote ya ubunge amefanya kazi ya kuiwajibisha serikali,” alisema.
 
Mafao  Yake
Alipotakiwa kuelezea kuhusu masilahi yake ya ubunge, Zitto alisema kwake masuala ya fedha halina nafasi kwa sababu yupo kwa sababu ya kusimamia masilahi ya Watanzania.
 
“Tangu mwaka 2011 nimekuwa mbunge pekee ambaye nimekuwa sipokei posho ya Bunge hadi naondoka bungeni kwa hivyo basi uamuzi wangu wa siasa hauangalii fedha bali hoja kwangu ni kuona tunapoelekea,” alisema.
 
Vigogo wajiunga
Wakati wa mkutano huo Zitto jana, chama hicho cha ACT-Tanzania, kilivuna wanachama wapya zaidi ya 10 wakiwamo waliokuwa viongozi wa Chadema katika ngazi ya mikoa na wilaya.
 
Waliojiunga na chama hicho ni pamoja na aliyekuwa mgombea ubunge wa kura za maoni CCM katika jimbo la Kasulu Mjini, Askofu Dk. Gerald Mpango, Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Haki za Binadamu Kanda ya Magharibi Chadema, Jaji Mstaafu Mussa Kwikima.
 
Mwingine ni Kansa Mbarouk aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Tabora, Jorum Mbogo aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kaliua, mgombea ubunge wa jimbo la Temeke mwaka 2010 Chadema, Dickson Ng’ili.
 
Wengine ni Meck Mzirai aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu, Charles Lubala Mwenyekiti wa jimbo la Kahama na mgombea ubunge 2010 Chadema na Diwani wa Mabogini Halmashauri ya Moshi, Albert Msando (Chadema).
 
Pia wamo Dk. Ben Kapwani aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Iringa, John Malaki Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Katavi, Mwasimtwa Mwagongo, Kaimu Mwenyekiti wa TLP Wilaya ya Mbarali na Katibu wa TLP Wilaya ya Mbarali, Selemani Nyumile.
  
Wabunge 10  Kujiunga  na  ACT
Akizungumza na Mwandishi  wetu  jana jijini Dar es Salaam, baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, Zitto alisema nyuma yake wapo wabunge zaidi ya 10, watakaojiunga na ACT muda sio mrefu.
 
“Siko mwenyewe wapo wenye mapenzi mema na tunataka kufungua ukurasa mpya kwa nchi yetu wa siasa za kujenga nchi, wabunge mahiri wa CCM na Chadema zaidi ya 10, watajiunga nami, ila sitakutajia majina kwa sasa kwa sababu ya sheria za vyama vyao, acha wamalizie vipindi vyao vya ubunge,” alisema Zitto .

Jumatano, 18 Machi 2015

Panya aliyemeza kipande cha dhahabu

Panya alimeza kipande cha dhahabu mwenye dhahabu akachanganyikiwa na kuamua kumkodi mpelelezi mmoja ili aje amuue panya aliyemeza dhahabu.
Mpelelezi alipofika alikuta panya zaidi ya 500 lakini alishangaa kumuona panya mmoja kajitenga,ndipo alipomkamata na kumuua,alipompasua akakuta kipande cha dhahabu akamkabidhi mwenyewe.Yule jamaa alipigwa na butwaaa huyu mpelelezi alimjuaje yule panya ikabidi amuulize.
Jamaa:aisee we mkali,ulijuaje kama huyu ndiye panya aliyemeza dhahabu?
Mpelelezi:hawa panya nao ni kama raia Watanzania wakiwa na mali hujitenga na wenzao.

Wadada wanashida

Taja vyakula vitatu unavyovipenda
Mwalimu katangaza test , Akatoa Masharti; Ukiandika jibu hamna kufuta au kukata.

Swali la kwanza,
Taja vyakula vitatu ambavyo ukienda hotelini umelipiwa utapenda kula (marks 1)

WAVULANA wakajaza; wali, ugali, mihogo.

WADADA wakajaza; burger, pizza, egg chop.

Swali la 2: Eleza jinsi ya kupika kila chakula ulichotaja hapo juu. (marks 99)

wacha wadada waanze kuhangaika kukata majibu ya mwanzo!!!

Jumanne, 17 Machi 2015

Aliyekuwa mwanasheria wa daktari wa ossama bin laden auawa.

liyewahi kuwa mwanasheria wa Daktari wa Osama bin Laden, Samiullah Afridi ameuawa kwa kupigwa risasi huko Pakistan. Mtu aliyekuwa na silaha


alimmshambulia Samiullah Afridi ambaye alikuwa ndani ya gari lake akiendesha eneo la Peshawar. Samiullah Afridi alikuwa mmoja wa wanasheria wa Dr.Shakeel Afridi ambaye ndiye aliyefichua siri kwa Marekani juu ya wapi alikokuwa Ossama Bin Laden ambaye alikuwa mafichoni huko Pakistani kwa takribani miaka minne. Dr Afridi wakati anauawa alikuwa katima matembezi alifungwa kifungo cha muda mrefu.Kundi la Talbani limekiri kutekeleza mauaji hayo.

Jumapili, 8 Machi 2015

Utajili wa zari kwisha habari yake, Diamond ashtuka

UTAJIRI WA ZARI KWISHA HABARI YAKE. DIAMOND ASHTUSHWA.


NI madai ya chini kwa chini kutoka vyanzo vilivyo karibu na mwanamuziki nyota nchini Uganda, Zarina Hassan ‘Zari The Bosslady’ ambaye kwa sasa ameshikamana kimapenzi na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwamba, utajiri anaoutangaza kuwa nao siyo kweli!Mwanamuziki nyota nchini Uganda, Zarina Hassan ‘Zari The Bosslady’.
Madai hayo yalilishangaza Risasi Jumamosi kiasi cha kutaka kusikia kwa kina kwa nini utajiri huo siyo wa kweli wakati Zari anaonekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa na mali zake, kama nyumba na magari?
MSIKIE HUYU
“Mimi ndiyo nawaambia. Zari kweli anajiwezaweza lakini si kwa mali anazozitangaza kuwa nazo. Mimi naishi Uganda, namjua vizuri sana Zari,” alisema mtoa habari huyo.
Risasi Jumamosi: “Twende polepole. Ina maana yale magari ambayo kwenye namba za usajili badala ya namba kumeandikwa ZARI GP, ZARI 3 GP, ZARI 1 GP, ZARI H GP na mengineyo mengi si ya kwake?”
Mtoa habari: “Mengine yake, mengine si yake.”
Risasi Jumamosi: “Kwa nini yawe si yake wakati yameandikwa Zari?”
Mtoa habari: “Kuna makampuni ya nje ambayo yakitoa magari yanaingia naye mkataba yeye ili kuyatangaza. Sasa kwenye mkataba Zari anatakiwa kubandika jina lake ili watu wajue staa mkubwa kama Zari naye anatumia magari kama yale.”
Moja kati ya magari ya kifahari anayomiliki.
KUHUSU NYUMBA?
Mtoa habari huyo alisema anavyojua yeye, Zari ana nyumba moja nchini Uganda na nyingine Afrika Kusini ambazo aliachiwa na mumewe wa ndoa, Ivan Ssemwanga wakati wanatengana.
“Ile nyumba alijenga akiwa na mume wake, Ivan, lakini Zari kama Zari hajajenga. Hata sehemu kubwa ya mali zake Zari mumewe ndiyo amefanikisha.”
VIGEZO VYA MADAI
Mtoa habari wetu alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, kwa uhalisia wa magari ya Zari yanaweza kufika ishirini jambo ambalo alisema haoni mantiki yake.“Zari anasema anamiliki shule, vyuo, magari na mahoteli, lakini ili avipate hivyo maana yake amefanya biashara za kumzalishia, si ndiyo? Sasa kwa mfanyabiashara wa kweli anaweza kununua magari ya kutembelea ya kifahari kumi na tano na yuko yeye na watoto wake watatu tu? Tena wadogo.
“Tabia ya mtu kununua kila gari la kifahari linaloingia ni ya wale watoto ambao baba zao ndiyo wenye mali. Lakini kwa mfanyabiashara anayetunza mtaji wake, hawezi kununua kila toleo la gari.


“Kama itatokea hivyo, basi atauza lile gari la mwanzo na kununua jingine. Matajiri wote duniani wana magari ya kifahari ya saizi ya familia. Anaweza kuwa nayo mengi lakini matumizi pia ni hivyohivyo, sasa Zari magari kumi na tano halafu yeye na wanae watatu, wadogo. Mimi nakataa jamani,” alisema mtonyaji huyo.
KUJA KWAKE BONGO
Mtu huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, kama Zari anamiliki zile Hammer ambazo bei ya chini kabisa moja ni kama shilingi milioni mia mbili, basi hata kuja kwake Bongo kumfuata Diamond, angekuwa na utaratibu huu:
“Kwanza, kwa utajiri anaosema anao, mjue pesa ina tabia ya kusema. Zari angekuwa akitaka kuja Bongo kumfuata Diamond, angekuwa anatanguliza gari lake moja la kifahari likiwa na dereva ambalo angekuwa akilitumia nchini halafu yeye angekuwa anafuata na ndege. “Sasa yeye anakuja na ndege, akifika anategemea kutumia BMW C6 la Diamond. Sidhani kama kwa utajiri anaoutangaza anao angekuwa anafanya hivyo,” alisema mtu huyo.
TURUDI KWENYE MADAI YA ZARI
Katika mahojiano na Kipindi cha The Sporah Show cha mtangazaji Sporah Njau nchini Uingereza,  Zari mwenye maskani yake Kampala na Afrika Kusini, alisema anamiliki ndinga kibao za kifahari zenye thamani kubwa.
MITANDAO YA UGANDA
Mitandao mbalimbali ya nchini Uganda, imebainisha kuwa Zari anamiliki BMW (2006) lenye thamani ya dola 47, 000 (Sh. milioni 75.2), Black Chrysler (2008) dola 16,000 (Sh. milioni 25.6) na Audi Q7 (2010) la dola 53,000 (Sh. milioni 84.8).
Mengine ni Silver Chrysler (2008) la dola 13,000 (Sh. milioni 20.8), Jetta Volkswagen (2006) linalomgharimu dola 27,000 (Sh. milioni 43.2), Mercedes Benz Convertible (2008) linalouzwa dola 26,000 (Sh. milioni 41.6) na Range Rover Sports (2010) lenye thamani ya dola 109,000 (Sh. milioni 174.4).
Pia ana Lamborghini Gallardo (2010) lililomgharimu dola 198,000 (Sh. milioni 316.8), Hummer H2 la dola 150,000 (Sh. milioni 240) na mengine mengi, yote yakiwa na jina lake badala ya namba za usajili.
KWENYE MAHOJIANO NA SPORAH
Zari alisema ana mjengo wa nguvu mjini Cape Town, Afrika Kusini na Apartments (nyumba za kupangisha na kila kitu ndani) jijini Kampala, Uganda.Jarida la Times la nchini Uganda linamtaja Zari kama mwanamke anayekaribia kuingia kwenye orodha ya wanawake matajiri Afrika.
DIAMOND ASHTUKA
Alipotafutwa Diamond na kuambiwa kwamba kuna habari utajiri wa Zari ni magumashi, alishtuka.
“Khaa zimetoka wapi hizo habari? Mbona mimi najua ni mali zake?” alisikika Diamond na kukata simu.
Jitihada za kumpata Zari ili aweze kuzungumzia utajiri wake hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kutopatikana hewani. Jitahada zinaendelea.

Jumanne, 3 Machi 2015

Dereva na masai

Baada ya kupanda daladala aina ya DSM kutoka Mbagala chalambe mpaka Mwenge na kulipa sh 500, Masai akachukua tax wakati wa kurudi, walipofika sasa shughuli ilikuwa hivi,

Masai: we dureva? Naulisa Ng’ombe na mbusi ipi ngali?
Dereva: Ni ng’ombe ghali Masai,
Masai: kwanini Ng’ombe ghali?
Dereva: kwa sababu ni mkubwa zaidi ya mbuzi
Masai: umepata..na mbusi na kuku ipi ghali?
Dereva: ni mbuzi kwa sababu nae ni mkubwa kuliko kuku,
Masai: Umepata..
Masai: sasa me nimekwenda kule mwenge kwa gari kubwa nikalitoa sh. 500 hii yako ndogo unasema nikupe 40,000 wewe acha wizi.. Nitakupa 250 Tu..wee acha ibia morani…

Orodha ya matajiri duniani

Orodha ya Forbes ya 2015 ya matajiri zaidi duniani.
1. Bill Gates $79.2bn (Microsoft)
2. Carlos Slim Helu $77.1bn (Mfanyibiashara Mexico)
3. Warren Buffett $72.7bn (Mfanyibiashara)
4. Amancio Ortega $64.5bn (Mwanzilishi wa maduka ya nguo ya Zara )
5. Larry Ellison $54.3bn (Kampuni ya teknolojia Oracle)
6. Charles Koch $42.9bn (Mfanyibiashara)
7. David Koch $42.9bn (Mfanyibiashara)
8. Christy Walton $41.7bn (mmiliki wa maduka ya Walmart)
9. Jim Walton $40.6bn (mmiliki wa maduka ya Walmart)

10. Liliane Bettencourt $40.1bn (Muuzaji wa vipodozi L'Oreal )

Jumatatu, 2 Machi 2015

Ingekuwa ni mkeo ungemfanya nini?

Jamaa karudi toka kazini mpole na hana furaha!

MKE; Vipi leo mbona mpole?
MUME; Ofisi yetu imeungua na watu wote waliokuwemo wamekufa.
MKE; Ilikuaje wewe ukapona?
MUME; Nilikua chooni jirani na ofisi najisaidia.
MKE; Loh maskini, familia zao itakuaje?
MUME; Watalipwa million 100 kila mfiwa.
MKE; KWA HASIRA, Ona sasa na wewe kunya kunya kwako umetukosesha mihela.. Ungeenda kunya akhera.

Je ungekuwa wewe ungemfanya nini huyo mwanamke?